Mahakama Kuu imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na
Wakili Onesmo Mpinzila pamoja na mambo mengine akipinga Kanuni za
Uchaguzi za Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) za mwaka 2016.
Kesi hiyo imetupiliwa mbali baada ya Mahakama kukubaliana na hoja
za mapingamizi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ndio
waliokuwa wadaiwa katika kesi hiyo.
Hoja hizo ambao Mahakama imekubaliana nazo ni pamoja na kwamba mdai
hakuwa na mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo na kwamba hati yake ya
kiapo kilichokuwa kikiunga mkono madai yake ilikuwa na kasoro za
kisheria.
Uamuzi huo umesomwa na Jaji Ignasi Kitusi kwa niaba ya jopo la
majaji watatu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo. Majaji wengine walikuwa
ni Rose Teemba(kiongozi wa jopo) na Beatrice Mutungi.

No comments:
Post a Comment