LATEST NEWS

Sunday, March 26, 2017

VISIMA VYA MAJI KUNUSURU NDOA NA MIGOGORO KWENYE FAMILIA KASOLOLO

KERO ya uhaba wa maji iliyokuwa ikiwakabili wananchi zaidi ya 1000 wa vitongoji vitano vya Kijiji cha Kasololo wilayani Misungwi mkoani Mwanza na kusababisha ndoa nyingi kuvunjika pamoja na migogoro kwenye familia, imetatuliwa baada ya Taasisi ya The Desk & Chair Foundation kuchimba na kujenga visima saba.
 

Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation tawi la Tanzania Sibtain Meghjee akikabidhi visima hivyo vilivyogharimu sh 21 milioni alisema walisitisha ujenzi wa Msikiti (nyumba ya ibada ) ili watatue kero ya maji kwa kuwapa wananchi huduma ya maji itakayowanufaisha watu zaidi ya 1200 kwa matumizi ya kibinadamu.

Alisema visima vimekabidhiwa ili kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Bi. Fatma AS. mjukuu wa Mtume Mohamed S.A.W.ambaye alifanya kazi kubwa ya kusaidia jamii lakini pia miradi ya kijamii inayofadhiliwa na waumini wa madhahebu ya Shia Ithna Asheri, kwenye maadhimisho hayo ilikabidhiwa huko Kwimba Mwanza na Kondoa mkoani Dodoma na maeneo mengine nchini.
Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation tawi la Tanzania Sibtain Meghjee akimtwisha ndoo ya maji milembe Kuhamwa, Mwenyekiti wa Kiyongoji cha Mwashileko katika Kijiji cha Kasololo wilayani Misungwi Mwanza, ikiwa ni ishara ya kukabidhi kisima cha maji safi na salama kati ya saba vilivyochimbwa na taasisi hiyo kwa gharama ya sh. 21 milioni.

No comments:

Post a Comment

Adbox