Gazeti moja Mexico linasema ghasia dhidi ya waandishi na kutoadhibiwa kwa wanaohusika na ghasia hizo zimesababisha kusitisha uchapishaji.
Katika tahariri, gazeti la Norte de Ciudad Juarez limesema nakala ya Jumapili ndiyo ya mwisho kuchapishwa.
Hatahivyo, gazeti hilo linasema litaendelea na shughuli zake katika mtandao.
Miroslava Breach, muandishi aliyelifanyia gazeti hilo kazi katika mji wa Chihuahua, alipigwa risasi na kuuawa mwezi uliopita.
Ni mmoja wa waandishi watatu waliouawa Mexico Machi.
Breach aliripotia magazeti ya Norte de Ciudad Juarez na La Jornada, gazeti la taifa mjini Mexico kwa mapana kuhusu uhusiano kati ya uhalifu wa kupangwa na wanasiasa katika jimbo la Chihuahua.
Alipigwa risasi mara nane ndani ya gari lake nje ya nyumba yake katika mji mkubwa kwenye jimbo hilo, Chihuahua.
Moja ya wanawe alikuwa ndani ya gari hilo lakini hakujeruhiwa.
Washambuliaji hao waliacha ujumbe kwenye karatasi unaosema: " kwa kuwa na mdomo mrefu."
Miroslava Breach ni muandishi wa tatu kuuawa Mexico mwezi Machi
Oscar Cantu, mhariri wa Norte de Ciudad Juarez amesema "Hakuna hakikisho wala usalama wa kuwa mwandishi asiye egemea upande wowote."
"Kila kitu maishani kina mwanzo na mwisho na malipo ya kulipa. Na iwapo malipo ni uhai wa mtu, siko tayari kwa washirika wenzangu kulipia hilo na mwenyewe pia siko tayari kulilipia hilo."
Waandishi 35 wameuawa Mexico kwasababu ya kazi zao tangu 1992 na robo ya idadi hiyo waliteswa pia, kamati ya kulinda waandishi inasema. Wengine watatu waliuawa wakiwa katika kazi hatari.
Katika wakati huo, waandishi 50 wameuawa katika matukio ambapo dhamira haikujulikana wazi.
Waandishi waliandamana kupinga mauaji ya Bi Breach
Mwezi uliopita, gavana wa jimbo la Chihuahua amesema serikali yake haina uwezo wa kukabiliana na uhalifu wa kupangwa.
Amesema ameiomba serikali kuu kusaidia polisi katika eneo lake kukabiliana na magengi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Source:Bbc Swahili
No comments:
Post a Comment