LATEST NEWS

Thursday, April 20, 2017

Gesi ya Mtwara kusambazwa Tanga, Morogoro

Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania linatarajia kufanya upembuzi yakinifu katika mwaka wa fedha ujao ili kuanza kuuza gesi itokayo Mtwara katika mikoa Tanga Morogoro na Dodoma.
Hayo yamebainishwa leo (Alhamisi) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Mhandisi Kapuulya Musomba ambaye amesema TPDC itafanya utafiti wa ujenzi wa miundombinu pamoja na masoko.
"Upembuzi huu ni kwa ajili ya kurahisisha taratibu za utekelezaji na kuratibu kazi ya usambazaji wa gesi nchi. Katika hili wawekezaji binafsi wanapaswa kushiriki katika ujenzi wa miundombinu," amesema Musomba.

No comments:

Post a Comment

Adbox