Klabu ya Simba jana iliibuka na kupinga utaratibu unaotumiwa
na TFF katika kushughulikia suala la pointi 3 ilizopewa kutoka klabu ya
Kagera Sugar kwa kosa la kumchezesha mchezaji aliyekuwa na kadi 3, huku
ikiituhumu TFF kuwabeba mahasimu wao, Yanga. Mkuu wa Idara ya Habari na
Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema wameshangazwa na kitendo
cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kupewa jukumu la
kushughulikia maombi ya Kagera Sugar ya kutaka mapitio ya maamuzi ya
Kamati ya Saa 72 kwani haina mamlaka hayo kwa mujibu wa utaratibu.
Manara amesisitiza kuwa lengo la TFF kulipeleka suala hilo kwenye kamati hiyo ni moja ya mbinu za kuhakikisha inaibeba Yanga katika mbio za ubingwa, na kwamba utendaji kazi wa kamati hiyo siku zote umekuwa si wa haki kwa upande wa Simba. Pamoja na hayo yote amemuomba Rais Magufuli kuingilia kati jambo hilo kwa kuwa mpira wa miguu umebeba dhamana kubwa kwenye mioyo ya watu pia kuwa na nguvu kubwa kuliko siasa kabla hawajaamua kufanya maamuzi mengine kutokana na kile wanachokiita kuwa ni hujuma wanayofanyiwa na TFF.

No comments:
Post a Comment