LATEST NEWS

Saturday, April 8, 2017

Kisukari Ni Ugonjwa Unao Weza Kudhibitiwa Kwa Kutumia Tiba Asilia





Kisukari ni tatizo la kiafya linalo wasumbua na kuwatesa mamilioni ya watu duniani. Miongoni mwa dalili za ugonjwa wa kisukari ni pamoja na

i. Kukojoa mara kwa mara ( Watoto kukojoa kitandani )

ii.Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.

iii.Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.

iv.Kupungua uzito kwa kasi au kukonda pamoja na kwamba unakula vizuri tena kila wakati kwa sababu ya kusikia njaa kila wakati kunakosababishwa na maradhi ya kisukari

v.Wanawake kupatwa na tatizo la kuwashwa ukeni.

vi.Kupoteza uwezo wa Kuona vizuri.

vii.Wanaume kupatwa na tatizo la ukosefu na / ama upungufu wa nguvu za kiume na wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa.

viii.Kupatwa na ganzi, kusikia hali ya kama kuchomwachomwa au kutohisi chochote pindi unapoguswa kwenye sehemu za miguu, viganjani na kwenye vidole.

ix.Miguu kuoza na hata kupata gangrini.

x.Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.

xi.Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.

xii.Kutokwa na Majipu kwenye sehemu mbalimbali mwilini.


Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu , watu walio katika makundi yafuatayo wapo katika hatari kubwa ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari kuliko watu wengine. Watu hao ni kama ifuatavyo :


i. Watu wenye uzito uliozidi,

ii.Watu wanao toka katika familia zenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari.

iii.Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,

iv. Watu wasio fanya mazoezi

v. Wagonjwa wa shinikizo la damu,

vi.Watu wenye kiasi kikubwa cha lehemu mbaya ( Bad Cholestrol ) kwenye damu.

vii.Watu wenye virimba tumo ( vitambi): Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa, kuna hatari kubwa ya kupatwa na maradhi ya kisukari ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu

viii.Watu wenye msongo wa mawazo na

ix.Watu wanao tumia pombe na kupita kiasi pamoja na wale wavutaji wa sigara kupita kiasi: Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kupatwa na tatizo la kisukari,kwani kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, uvutaji sigara huathiri moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu. Tafiti mbalimbali za kiafya zinaeleza kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.

x. Kundi jinginge la watu walio katika hatari ya kupatwa na maradhi ya kisukari ni watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 55 na kuendelea

Wataalamu wa afya wanashauri watu walio kwenye orodha iliyo tajwa hapo juu, kujiwekea utaratibu wa kuwa wanapima afya zao walao mara moja kila mwakaili waweze kuchukua hatua stahiki za kiafya endapo watakutwa na tatizo la sukari.

Image result
TIBA ASILIA KWA WAGONJWA WA KISUKARI
Zipo tiba asilia mbalimbali zinazo saidia kkupunguza maradhi ya kisukari. Miongoni mwa tiba hizo ni pamoja na tiba ijulikanayo kama Mkatasukari. Tiba hii inasaidia kushusha na kudhibiti kiwango cha sukari kwa mgonjwa mwenye sukari ya kupanda. Kama unasumbuliwa na maradhi ya kisukari ( Sukari ya kupanda ), unaweza kujaribu kutumia tiba hii.

JINSI YA KUANDAA TIBA ASILIA YA MKATASUKARI

Mahitaji ;
i. Nanasi moja kubwa

ii. Majani ya chai vijiko vitatu vya chakula

iii. Maji lita tano

iv. Dawa asilia ya Mkatasukari vijiko vikubwa vitatu.


MATAYARISHO: Chukua nanasi lako lililo iva vizuri, limenye kisha likate vipande vidogo vidogo, kisha liweke kwenye sufuria halafu ndani ya sufuria hilo, ongeza lita tano ya maji safi. Baada ya hapo weka majani ya chai vijiko vikubwa vitatu, kisha ongeza vijiko vikubwa vitatu vya dawa asilia ya Mkatasukari, kisha chemsha kwa muda wa dakika thelathini (30).

Baada ya dakika thelathini, ipua na uchuje, makapi weka pembeni, kisha hifadhi kimiminika chako kwenye chombo safi.


MATUMIZI :
Tumia kunywa kikombe kidogo chenye ujazo milimita mia mbili na hamsini ( 250 mills ) au robo lita kwa lugha nyepesi. Utafanya hivyo mara tatu kwa siku, asubuhi mchana na jioni hadi dozi yako itakapo kamilika.

Baada ya kutumia dozi hii, unashauriwa kwenda hospitali kupima tena sukari ili ujue sukari yako imeshuka kwa kiasi gani pamoja na kupata ushauri wa daktari wako.

Kwa mahitaji yako ya tiba asilia ya Mkatasukari, fika katika duka la NEEMA HERBALIST. Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA.

Kwa wateja wetu waliopo jijini DAR ES SALAAM, ambao hawawezi kufika ofisini kwetu., tunatoa huduma ya kuwapelekea dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ), kwa wateja waliopo Zanzibar watasafirishiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti, kwa wateja waliopo mikoani watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa mabasi mbalimbali. Wateja waliopo NAIROBI na MOMBASA watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa mabasi mbalimbali.






No comments:

Post a Comment

Adbox