LATEST NEWS

Saturday, April 8, 2017

Kagera Sugar yaahidi kuendeleza ubabe kwa JKT Ruvu

  
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime amesema, amekipanga kikamilifu kikosi chake kuhakikisha wanawaangamiza JKT Ruvu kwa kuvuna pointi tatu ili kuchochea azma yao ya kumaliza msimu wakiwa katika nafasi tatu za juu.

Mecky amesema, anaamini ushindi wao katika mchezo dhidi ya Simba utakuwa kichocheo cha cha timu yake kuitungua JKT Ruvu katika mchezo huo.

"Nashukuru kuona timu yangu inazidi kupata mafanikio, haya ni matunda yanayotokana na mipango tuliyojiwekea toka awali, lengo letu kwa sasa ni kuona tunashinda michezo yetu iliyosalia ili tumalize ligi tukiwa kwenye nafasi tatu za juu," alisema Mexime

Kocha huyo wa Kagera Sugar Mecky Mexime amesema anaamini mpaka sasa nafasi ya Ubingwa ipo kwa timu yoyote iliyonafasi za juu.

"Mpaka sasa nafasi ya ubingwa ipo wazi na lolote linaweza kutokea kwa timu yoyote kutwaa ubingwa wa msimu huu," alisisitiza Mexime

No comments:

Post a Comment

Adbox