KIUNGO wa Simba SC Mzamiru Yassin ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa
mwezi wa tatu (March) ya timu ya Simba, katika Mwezi wa tatu Simba
ilicheza mechi tano ikiwa mechi mbili ni za mashindano ilicheza na Mbeya
City kwenye ligi kuu, wakacheza na Madini Fc katika kombe la
shirikisho Azam Sports Federation Cup (ASFC) na mechi tatu za kirafiki
dhidi ya (Polisi Dodoma, Chemba Kombaini, na Mererani Kombaini) .
Simba imekuwa na utaratibu mzuri wa kumchagua mchezaji yoyote
ambae alionyesha kiwango safi na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri
na kumtunuku tuzo hiyo kama hamasa kwa wengi kufanya vizuri ili
kufanikiwa kuipata tuzo hiyo.
Wachezaji
wengine ambao wameshanyakua tuzo hiyo ni Abdi Banda mwezi wa pili,
Laudit Mavugo mwezi wa Kwanza. Hii ni Mara ya pili kwa Mzamiru Yassin
kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi kwa timu ya Simba.
Saturday, April 29, 2017
MCHEZAJI BORA MARCH MZAMIRU YASSIN
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment