LATEST NEWS

Thursday, April 27, 2017

Migodi yalalamikiwa kwa udhalilishaji, yapekua wafanyakazi maungoni

Bunge limeelezwa kuwa, baadhi ya wamiliki wa migodi huwapekua wafanyakazi hadi sehemu za siri ili kubaini iwapo wameficha madini. Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Joyce Mukya akiuliza swali leo bungeni alisema kumekuwa na vitendo vya udhalilishaji kwa wafanyakazi wa migodini kwa kupekuliwa hadi sehemu za siri na wenye migodi. “Kumekuwa kunafanyika udhalilishaji mkubwa kwa wafanyakazi, wamekuwa wakikaguliwa sehemu za siri hasa njia ya haja kubwa, je, Serikali inatuambia nini na inachukua hatua gani juu ya udhalilishaji huu?” alihoji Mukya. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde akijibu swali hiyo alisema malalamiko hayo aliyapata katika mgodi wa TanzaniteOne hivyo wanayatambua.

No comments:

Post a Comment

Adbox