KRC Genk waliingia uwanjani kucheza mchezo huo wakiwa wana rekodi ya kuwa timu pekee katika timu 12 zinazocheza mechi hizo kutofungwa mchezo hata mmoja wakiwa wameshinda michezo yote minne, hata hivyo jana wakiwa ugenini wamelazimishwa sare ya 1-1 na kuwafanya kupata sare ya kwanza.
AS Eupen licha ya kuwa nyumbani walianza kufungwa goli dakika ya 20 mchezaji Malinovsky akipachika goli la kwanza la Genk lakini AS Eupen walisawazisha goli hilo dakika ya 51, katika michezo ya mtoano KRC Genk na AS Eupen ndio timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo katika timu 12 za Kundi A&B lakini AS Eupen wameshinda mechi moja pekee kati ya tano.
No comments:
Post a Comment