LATEST NEWS

Thursday, April 13, 2017

Mmea Hatari:Magugu Karoti Yavamia Nchi



Mkurugenzi Wa Taasisi ya ECHO inayojishughulisha na utafiti Wa kilimo na kupunguza njaa ndugu Erwin Kinsey ,akitoea elimu kwa waandishi Wa habari juu ya gugu Karoti.
Waandishi wa habari jiji Arusha wamepewa Elimu na kutakiwa kuielimisha jamii isiyo fahamu Kufuatia tishio la mmea hatari unaofahamika kwa jina la gugu karoti katika lugha ya kitaalam (Partheniun) unaoadhiri afya za binadamu,mifugo na mazingira na na jamii kutofahamu hasa wakulima na wafugaji

Elimu hiyo imetolewa katika semina iliyowakutanisha waandishi wa habari na Shirika linaopambana na kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji kuhusu mmea huu hatari ECHO EAST AFRICA jijini Arusha

Akizungumzia madhara ya mmea huo kwa binadamu na wanyama mkurugenzi wa shirika la ECHO ndg ERUWINI KENZI amesema kuwa Mmea huo umesambaa maeneo mengi nchini ikiwemo Arusha ,Kilimanjaro na Manyara

Kwa upande wake bwana shamba bwana chalse Bony amesema watu wengi wanatumia majani haya bila kufahamu na kusababisha madhara MAKUBWA kwa afya zao wanatumia kama mafagio,kama maua na kuwaomba waandishi ,wazazi kuelimisha watu kufahamu madhara ambayo yanasababishwa na zao hilo

Mnyama akila majani hayo anaweza kufa na pia maziwa yake yanakuwa machungu yenye uchachu na yanaleta madhara kwa mtumiaji,kwa kuku haiwezi kuendelea kutaga tena.

Asili ya mmea huo umetokea nchini Mexico ,uligundulika miaka ya 1960 ambapo mmea mmoja unauwezo wa kuzaa mbegu 25,000 kwa mche mmoja.

No comments:

Post a Comment

Adbox