Jeshi la
polisi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuteketeza ekari 17 za zao la bangi
katika kata ya Kisimiri juu wilayani Arumeru mkoani Arusha na kutoa onyo kali
kwa wananchi ambao wanaendelea na biashara hiyo.
Hayo
yamethibitishwa na kamanda wa polisi mkoani hapa kamanda Charles Mkumbo ambapo
ameeleza kuwa waliweza kufanya msako katika kata ya Kisimiri juu na kufanikiwa
kuteketeza jumla ya ekari 17 za zao hilo ambapo kamanda Mkumbo amweataka
wananchi wa kata hiyo kuacha tabia ya kulima zao hilo kwani kufanya hivyo ni
kinyume na sheria.
Baadhi ya
watuhumiwa wa kilimo cha zao hilo wamekuwa wakikimbilia mlimani pindi
wanapobaini jeshi la polisi kuingia katika kata yao ambapo hapa kamanda mkumbo
akatoa kauli yake kwa watu hao.
No comments:
Post a Comment