LATEST NEWS

Thursday, April 13, 2017

Mwigulu asema wizara yake haitaruhusu uhalifu kuendelea nchini

 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba imesema wizara yake hatoruhusu uhalifu wa aina yeyote kuendelee kutokea nchi na badala yake wizara yake itaendelea kulinda na kutetea usalama wa raia na mali zao.

Mwigulu ametoa kauli hiyo wakati akijibu hoja za wabunge katika makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge kwa mwaka 2017/2018.

Aidha Waziri Mwigulu amewataka watu wote wenye mahojiano maalumu na wabunge kuwafuata wabunge hao Dodoma badala ya kuwaondoa na kwenda kufanya nao mahojiano nje ya Dodoma.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amewasihi wabunge kuviacha vyombo vya ulizi na usalama kufanya yake.

Naye Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kwa mwaka ujao wa fedha serikali imetenga Shilingi Bilioni 60 kwa ajili ya kupeleka fedha kila kijiji ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala.

BERTHA MWAMBELA

No comments:

Post a Comment

Adbox