LATEST NEWS

Thursday, April 13, 2017

Baraza la watoto Tanzania laongeza nguvu dhidi ya udhalilishaji wa watoto

 
Rais wa Baraza la watoto Tanzania Ameir Haji amesema katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto wameweza kupiga hatua ya kuunda mabaraza ya watoto kila wilaya ambayo yatashirikiana katika kupaza sauti zao kukemea ukatili kwa watoto nchini.

Akizungumza katika uzinduzi wa jengo la kituo cha haki za watoto Mazizini amesema ipo haja kwa serikali na taasisi binafsi kuzidisha jitihada katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa watoto ili kuzitokomeza kabisa kesi hizo hapa Zanzibar.

Nae Katibu mkuu wa jumuiya ya haki za watoto Zanzibar Jamila Mohammed Juma amesema ipo haja ya kuungana kwa pamoja kati yao na watoto katika kutetea haki za watoto katika kumlinda na udhalilishaji ikiwa na lengo la kukiondoa kilio cha mda mrefu kwa watoto wanaofanyiwa ukatili.

Kwaupande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uwezeshaji,Vijana,Wazee,Wanawake na Watoto Hassan Khatib Hassan amesema serikali imedhamiria kuweka nguvu zake zote kupambana na udhalilishaji wanaofanyiwa watoto na kuwataka watoto nchini kutoa taarifa katika mamlaka husika pindi watakapofanyiwa ukatili wa aina yoyote katika jamii.

No comments:

Post a Comment

Adbox