Wajumbe wa Chama cha Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu kutoka nchi 54 za Afrika wamekutana mjini Abidjan, Cote d’Ivoire, wakijadili jinsi ya kutatua na kukabiliana na mgogoro wa njaa unaoikumba Afrika.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huu, naibu mwenyekiti wa shirikisho la kimataifa la vyama vya msalaba mwekundu na hilali nyekundu Bw. Abbas Gullet amesema, hivi sasa, bara la Afrika linakabiliwa na matatizo mengi, lakini njaa ni suala kubwa linalowatishia maelfu ya waafrika.
Naye mwenyekiti wa chama cha msalaba mwekundu cha Cote d’Ivoire Souare Karidiata Koné amesema mkutano huo utajadili jinsi ya kufanya msaada wa kimataifa ukidhi mahitaji halisi ya walengwa na kuongeza nguvu ya shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na hilali nyekundu katika kuzisaidia idara husika za serikali.
No comments:
Post a Comment