LATEST NEWS

Tuesday, April 11, 2017

Waziri mkuu amkabidhi cheti cha uteuzi mkuu wa Hong Kong

 
Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amemkabidhi cheti cha uteuzi Bi. Lam Cheng Yuet-ngor, atakayeshika wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa tano wa Mkoa wa Utalawa Maalumu wa Hong Kong kuanzia Julai Mosi.

Amesema serikali kuu itamuunga mkono kikamilifu mkurugenzi mkuu huyo na serikali ya Hong Kong katika kuendeleza uchumi, kuinua kiwango cha maisha ya watu na kuhimiza mawasiliano na ushirikiano na China bara.

Wakati huohuo, rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing pia amekutana na Bi. Lam Cheng Yuet-ngor na kumtaka aongoze awamu mpya ya serikali ya Hong Kong, kuunganisha watu wa sekta mbalimbali mkoani humo, kutekeleza kwa ukamilifu na usahihi sera ya “China Moja na Mifumo Miwili” na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya Hong Kong.


No comments:

Post a Comment

Adbox