LATEST NEWS

Monday, April 10, 2017

Rais Magufuli ateua kamati ya pili ya kuchunguza mchanga wa madini

 
Rais Dkt. John Magufuli amewateua wajumbe wa kamati maalumu ya pili itakayochunguza madini yaliyomo kwenye mchanga uliopakiwa wenye makontena katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kamati hiyo inajumuisha wajumbe wanane ambao ni wachumi na wanasheria na imetanguliwa na kamati ya kwanza iliyoundwa na wataalamu wa masuala ya jiolojia, kemikali na uchambuzi wa kisayansi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu kutoka kwa Katibu Mkuu  Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa. Prof. Nehemiah osoro Prof. Longinus Rutasitara, Dkt. Oswald Mashindano, Gabriel Malata, Casmir Kyuki, Butamo Philip, Usaje Usubisye na Andrew Massawe.

Wajumbe hao wataapishwa kesho  Ikulu Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Adbox