LATEST NEWS

Friday, April 21, 2017

REAL MADRID NA ATLETICO MADRID, JUVE NA MONACO NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA


Wapinzani wa jiji la Madrid, Real Madrid na Atletico Madrid watakutana katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.


Nusu fainali nyingine itakuwa kati ya Juventus ya Italia na Monaco.
Katika marudio ya fainali ya msimu uliopita, mahasimu hao wa La Liga watakutana Uwanja wa Bernabeu Mei 2 na mchezo wa marudiano utafanyika Uwanja wa Vicente Calderon.

Monaco watakuwa wenyeji wa mabingwa wa Serie A, Juventus Uwanja wa Louis II Mei 3 kabla ya kusafiri kwenda Turin kwa mchezo wa marudiano Mei 10.
Uwanja wa Cardiff ndiyo utakaohodhi fainali ya michuano hiyo Juni 3, hiyo ikiwa mara ya kwanza mfalme wa Ligi ya Mabingwa anapatikana katika ardhi ya Wales.

Unakumbuka jinsi Simeone alivyofungwa na Real Madrid mara mbili katika fainali za Champions League? Pengine ni kati ya suala ambalo Simeone hataki kulikumbuka kabisa.

Lakini sasa amepewa nafasi ya kulipa kisasi kwani katika droo ya Champions League iliyofanyika mchana huu majirani hao wawili kutoka mji wa Madrid wanakutana katika nusu fainali ya Champions League

Atletico ambao walifika katika hatua hii baada ya kuwaondoa mabingwa wa soka wa nchini Uingereza klabu ya Leicester City wanakutana na Real Madrid ambao nao waliiondosha kwenye michuano hii miamba ya Ujerumani klabu ya Bayern Munich.

Tayari watu wameshaanza kuusubiri mchezo huu kwa hamu kubwa haswa wakikumbuka fainali ya mwaka 2014 na ile ya 2016 ambazo ziliwakutanisha Madrid na Atletico huku zote Madrid wakiibuka kidedea

Nusu fainali nyingine itakuwa kati ya Monaco ambao msimu huu hawashikiki watakaokutana na timu ngumu zaidi kufungika katika mashindano haya ya msimu huu,klabu ya Juventus kutoka nchini Italia.

Monaco wanaingia katika nusu fainali hii wakijiamini kutokana na kuwa na safu ya ushambuliaji kiwembe ambapo Mbappe na Falcao wamekuwa wauaji wa nyavu lakini wakikutana na ukuta mgumu wa Juventus ambao waliwatoa Barcelona katika hatua ya robo fainali.

Nusu fainali ya kwanza itapigwa tarehe 2 na 3 mwezi wa 5, kabla ya michezo ya marudiano itakayopigwa tarehe 9 na 10 ya mwezi huo huo wa tano.





No comments:

Post a Comment

Adbox