LATEST NEWS

Friday, April 21, 2017

Waliowatoa kina Samata waingia anga za “Mashetani Wekundu”


Baada ya kuwafungasha virago kina Mbwana Samata na klabu yake ya Genk, sasa klabu ya Celta Vigo imeangukia mikononi mwa Manchester United katika nusu fainali ya michuano ya Europa League.

United ambao msimu huu hawana uhakika wa kuingia katika top four ya ligi kuu Uingereza inawalazimu kufanya kazi kubwa katika mashindano ya Europa kwani wakibeba kombe hilo watafudhu Champions League kama mabingwa wa Europa.

Lakini hii inaonesha huenda pengine kama Genk wangefanikiwa kuwatoa Celta Vigo baasi leo Genk ndio wangepangwa na Man United na hivyo kutimia kwa ndoto ya Samata ya kukipiga na Man United, lakini bahati haikuwa yao.

Huu unaweza kuwa mtihani mgumu kwa Celta Vigo kuwazuia United, japokuwa United nao wanapaswa kuwa makini na Celta Vigo ambao wana rekodi nzuri katika mechi zao za ugenini za Europa msimu huu.

Lyon nao baada ya ushindi mgumu dhidi ya Besitkas watapambana na Ajax kutoka nchini Uholanzi katika nusu fainali nyingine ya michuano hiyo ya Europa, Ajax waliingia katika hatua hii ya nusu fainali baada ya kuwatoa Schalke 04 kutoka nchini Ujerumani.

Nusu fainali ya michuano hiyo inatarajia kupigwa tarehe nne mwezi ujao, kabla ya timu hizo kurudiana tarehe 11 mwezi huo huo wa tano.

No comments:

Post a Comment

Adbox