Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake ni jambo la kawaida huku akisitiza kuwa hayajaanza kutokea leo kwani ni tukio kama matukio mengine.
Kamanda Sirro amesema hayo baada ya kelele za watu kwenye mitandao ya kijamii ndani ya siku tatu, huku wasanii, wanasiasa pamoja na wadau mbalimbali wa muziki kuja juu juu ya suala la kupotea vijana hao katika mazingira ya kutatanisha huku wengine wakihusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa yanayoendelea nchini.
“Matukio ya utekaji hayajaanza leo, hili la kina Roma na wenzake ni tukio kama matukio mengine yaliyokuwa ya ujambazi kwa hiyo tupeni muda tupeleleze, tukifika mahali pazuri tutawaita tuwape taarifa lakini nimeona mitandao mingi inazungumza, jana nikaona wasanii wamekutana lakini nikajiuliza hivi yangekuwa haya matukio yanatokea ya uhalifu yanapotokea watu wanakutana ingekuwaje ?,Jamani kazi hii tumepewa kwa mujibu wa Katiba na ni lazima tutimize wajibu wetu kwa hiyo tupeni muda tutakuwa na majibu mazuri katika hili”. Alisema Kamishna Sirro pindi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisni kwake Jijini Dar es Salaam
Aidha Kamanda huyo amesema mpaka sasa wameshaunda timu ya uchunguzi na inaendelea vizuri katika upelelezi huku akiwataka wananchi kuwa na subra kwa kuwa upelelezi ndiyo utasema kila kitu.
Kwa upande mwingine amewataka watu waache tabia ya kujifanya wao ndiyo ‘Kamishna Sirro’ na kutaka kuzungumzia habari za upelelezi hivyo amewataka watu kuliamini jeshi la Polisi kwa kuwa hawapendi vitendo hivyo viwepo na viendelee kutokea.
Source:EATV
Saturday, April 8, 2017
Sakata la kina Roma ni jambo la kawaida - Sirro
Tags
# BURUDANI
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
BURUDANI
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment