LATEST NEWS

Tuesday, April 18, 2017

TAASISI YA NAMELOK KUJENGA KITUO CHA ELIMU KWA AJILI YA WAJASILIAMALI WASICHANA WILAYANI KIBAHA MKOANI PWAN


KATIKA
kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano kupambana na wimbi la umasikini taasisi ya Namelok ya Wilayani Kibaha inatarajia kujenga kituo maalumu cha wasichana na wanawake wajasiriamali ambacho kitakuwa kinajihusisha na masuala ya utoaji wa mafunzo mbali mbali kwa lengo la kuweza kuwapa fursa ya kuachana na kuwa tegemezi na kujiajiri wao wenyewe.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho zilizofanyika katika Kata ya Mwendapole iliyopo katika halmashauri ya mji wa Kibaha Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Janet Mwasuka amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa kuwainua wanawake hao kiuchumuni kupitia mafunzo ya stadi za kazi pamoja na fursa zilizopo kutokana na elimu watakayoipata.

Janet alibainisha kuwa anatambau kuwa wanawake wegine katika Wilaya ya Kibaha ambao baadhi yao wameshindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa elimu ya ujasiriamali hivyo ana imani kituo hicho kitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wanawake pamoja na jamii yote kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Purple Planet ya Jijini Dar es Salaam inayojishughulisha na kuwasaidia katika kuendesha biashara zao na kuwainua kiuchumi wanawake wajasiriamali Hilda Kisoka amebainisha kuwa mikakati yao waliyojiwekea ni kufika mbali zaidi na kuuza bidhaa wanazozizalisha hapa nchini hadi nje ya nchi kwa lengo la
kujitangaza zaidi.

Alisema kwamba ana imani wanawake wengi hapa nchini wana uwezo mkubwa wa kuengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu hivyo ameiomba serikali ya awamu ya tano kuwasaidi kwa hali na mali ili kuweza kufika mbali katika kuleta ushindani zaidi wa masoko katika nchi zingine za nje na kuondokana na kuwa tegemezi.

No comments:

Post a Comment

Adbox