Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wafanyakazi16 wa Kampuni ya Quality
Group, kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya jumla ya sh. Milioni 22.
Washtakiwa hao wametiwa hatiani baada ya wiki iliyopita kukiri mashtaka yao mahakamani hapo.Katika Hukumu hiyo, washtakiwa kila mmoja amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu
katika kila kosa au kulipa faini ya sh. Milioni 1.5 kila mmoja katika kila kosa katika makosa matatu.
Washtakiwa hao walikuwa wanatuhumiwa kwa mashtaka matano likiwemo la kufanya kazi nchini kinyume na sheria na kuzuia maofisa Uhamiaji kutimiza majukumu yao.
Washitakiwa wote wametiwa hatiani leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.Hata hivyo, washitakiwa hao waliachiwa huru baada ya kulipa faini hiyo na kukwepa kifungo hicho.
Washitakiwa katika kesi hiyo ni Jose Kiran (40), Prakash Bhatt (35) ambao kwa pamoja walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya kuzuia maofisa wa Uhamiaji kufanya kazi yao.
Wengine ni Rajat Sarkar (35), Jagadish Mamidu (29), Niladri Maiti (41) Divakar Raja (37) ambao ni washauri wa kampuni hiyo, huku Mohammad Shaikh (44) mhasibu na Pintu Kumar (28) ambaye ni Meneja msaidizi wa kampuni.
Wengine ni, Bijenda Kumar (43), Prasson Mallik (46), Nipun Bhatt (32), Anuj Agarwal (46), Varun Boloor, Arun Kateel (46), Avinash Chandratiwari (33) na Vikram Sankhala (50)
wote walikuwa wanakabiliwa na mashitaka matatu ya kukutwa na visa za kughusho na kufanya kazi nchini kinyume cha sheria
Hakimu Mkeha amesema, washitakiwa 14 kila mmoja atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni
1.5 kwa makosa matatu huku washitakiwa wawili wote kwa pamoja faini ya Sh milioni moja kwa kosa moja.
Imedaiwa kuwa, Februari 20, mwaka huu washitakiwa Jose Kiran, na Prakash Bhatt waliwazuia maofisa uhamiaji kutimiza majukumu yao baada ya kukataa kuripoti kwa Ofisa
Uhamiajiwa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kujaribu kukimbia nje ya nchi kupitia mpaka wa Horohoro.
Ilidaiwa kuwa kwa washitakiwa 14 wanadaiwa kutenda kosa hilo Februari 13 mwaka huu maeneo ya Kampuni ya Quality Group wilayani Ilala mkoa wa Dar es Salaam.
Imedaiwa kuwa washitakiwa wote wakiwa ni raia wa nchini India, walikutwa na visa
zilizoghushiwa kinyume na kifungu namba 31 (1) (e) na kifungu namba 2 cha sheria ya uhamiaji ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho na sheria namba 8 ya mwaka 2015.
Iliendelea kudaiwa kuwaalidai katika mashitaka ya pili kuwa washtakiwa hao walikutwa wakiishi nchini kinyume na sheria.Aidha katika shtaka la tatu, washtakiwa hao walikutwa wakifanya kazi nchini kinyume cha sheria.
Tuesday, April 18, 2017
Home
/
HABARI MBALIMBALI
/
wafanyakazi 16 wa Kampuni ya Quality Group wahukumiwa kwenda jea miaka mitatu au kulipa faini.
wafanyakazi 16 wa Kampuni ya Quality Group wahukumiwa kwenda jea miaka mitatu au kulipa faini.
Tags
# HABARI MBALIMBALI
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
HABARI MBALIMBALI
Labels:
HABARI MBALIMBALI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment