LATEST NEWS

Monday, April 10, 2017

TMA: Mvua kubwa kunyesha usiku wa leo Jumatatu hadi Jumatano

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa Watanzania juu ya kuendelea kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia leo Jumatatu hadi Jumatano.
“Mvua hii yenye wastani wa asilimia 60, inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua nchini,” imesema taarifa hiyo.
 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyoitoa leo (Jumatatu), mamlaka hiyo imesema kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24.
Mamlaka hiyo imesema mikoa itakayoathirika ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Kutokana na hali hiyo, mamlaka imewataka wakazi mikoa hiyo kuchukua hatua stahik

No comments:

Post a Comment

Adbox