Mwenyekiti wa kamati ya Umoja huo Bw. Moussa Faki Mahamat ameeleza wasiwasi wake kuhusu ongezeko la mapambano ya kijeshi hasa katika eneo la Upper Nile.
Bw. Mahamat ameyataka serikali ya mpito na makundi ya upinzani nchini humo yasimamishe mara moja mapigano yanayotishia usalama na maisha ya raia nchini humo.
Ameongeza kuwa mapigano mapya yaliyoibuka nchini humo yameonesha kwamba pande husika zinaendelea kuamini utatuzi wa kijeshi na kupuuza machungu ya raia wa kawaida ambao wanadai kuwawakilisha na kuwalinda.
No comments:
Post a Comment