Waziri wa Katiba na Sheria amewasilisha maombi ya kuwasafirisha washitakiwa watatu akiwemo Ally Hatibu Hassan maarufu kama Shkuba kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kujibu tuhuma za kusafirishaji dawa za kulevya.
Washitakiwa wengine ambao wanaungana na Shkuba ni Idd Mafuru na Lwitiko Emmanuel Adam.
Maombi hayo yamewasilishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya kifungu namba 5 (1) cha Sheria ya Usafirishaji wahalifu sura ya 368 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Katika maombi hayo upande wa waziri kupitia DPP wanaiomba mahakama hiyo isikilize ushahidi na itoe amri ya kuwahifadhi washitakiwa ndani wakiwa wanasubiri kibali cha Waziri huyo cha kuwasafirisha nje ya nchi kwa mashitaka hayo.
Source:Michuzi
No comments:
Post a Comment