Wapiganaji Sudan Kusini, na silaha hatari
Afisa mmoja wa kundi la waasi na kasisi mmoja wa kanisa Katoliki, wanasema kuwa idadi kubwa ya watu wameuwawa katika mji wa Wau nchini Sudan Kusini, kwa sababu ya kabila lao.
Muasi huyo Dominic Ukello, amesema kuwa majeshi ya serikali na kundi moja la wapiganaji linaloshirikiana na serikali, wamekuwa wakiwalenga watu wa makabila madogo madogo, ambao wanaonekana kuwaunga mkono waasi.
Anasema kwamba, wamekuwa wakilipiza kisasi baada ya makamanda wawiwili walipouwawa na wapiganaji waasi.
Naye kasisi Moses Peter, amesema kuwa zaidi ya watu 5,000 walikuwa wamekimbilia usalama wao ndani ya jengo la kanisa Katoliki huko Wau.
Msemaji mmoja wa jeshi, anaripotiwa akisema kuwa, mapigano mjini Wau, yalianza baada ya askari wa gereza lililoko mjini humo, kugoma na kuasi.
Source:Bbc Swahili
Monday, April 10, 2017
Mauwaji ya kikabila yatokea Mjini Wau, Sudan Kusini
Tags
# KIMATAIFA
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
KIMATAIFA
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment