LATEST NEWS

Tuesday, April 18, 2017

WATU TISA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUVUNJA NYUMBA USIKU NA KUIBA MALI WILAYANI ILEMELA.

 
WATU TISA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUVUNJA NYUMBA USIKU NA KUIBA MALI WILAYANI ILEMELA.

KWAMBA KUANZIA TAREHE 09.04.2017 MAJIRA YA SAA 23:00HRS USIKU NA KUENDELEA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KUMEFANYIKA MISAKO NA DORIA YA KUWASAKA WATU WANAOJIHUSISHA NA UVUNJAJI WA NYUMBA USIKU NA KUIBA MALI AMBAPO WATU TISA WAMEFANIKIWA KUKAMATWA.

WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WANAFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.THIMOTH PAUL MIAKA 53, MKAZI WA KILIMAHEWA, 2 SANDRU SELEMAN MIAKA 24, MKAZI WA GHANA, 3.AHMED BAJBER MIAKA 27, MKAZI WA KILIMAHEWA, 4.JOSEPH KICHONGE MIAKA 28, MKAZI WA UHURU, 5.VICTOR SYLVESTER MIAKA 28, MKAZI WA IGOMBE, 6.ELIAS SAMWEL MIAKA 35, MKAZI WA MECCO, 7.DAMALI SAMWEL MIAKA 29, MKAZI WA ISENYI, 8.DAUD JAMES MIAKA 20, MKAZI WA MECCO, NA 9.PROCHES SAMWEL MIAKA 20, MKAZI WA KIGOTO.

KATIKA OPERESHENI HIYO ASKARI WALIFANIKIWA KUKAMATA MALI/VITU MBALIMBALI AMBAVYO WATUHUMIWA WALIKAMATWA NAVYO AMBAVYO NI, FLAT TV TATU, MBILI AINA YA LG ZA INCHI 32 NA 47 NA MOJA AINA YA SUMSUNG YA INCHI 32, RADIO MOJA AINA YA SABUFA PAMOJA NA SPIKA ZAKE MBILI, HOME THIETA MOJA, RADIO NDOGO MOJA AINA YA AITKESON NYEUSI, LAPTOP TATU YA KWANZA AINA YA DELL, YA PILI AINA YA HP NA YA TATU AINA YA LENOVO, BEGI LENYE NGUO MBALIMBALI, MONITOR AINA YA DELL NA CPU AINA YA DELL.

AIDHA MAENEO AMBAYO ASKARI WALIFANYA OPERESHENI BAADA YA KUPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA NI KATA YA KIRUMBA KATIKA MAENEO YOTE YA SOKO LA KIRUMBA, KATA YA KITANGIRI, KATA YA NYAMANORO, KATA YA PASIANSI, KATA YA IBUNGILO, NA KATA YA KAWEKAMO, AIDHA BAADHI YA VITU/ MALI ZILIZOKAMATWA TAYARI ZIMEWEZA KUTAMBULIWA NA WAMILIKI WA MALI HIZO.

WATUHUMIWA WOTE WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, AIDHA UPELELEZI NA MISAKO YA KUWAKAMATA WAHALIFU WA AINA KAMA HII BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU NA UHALIFU MAPEMA ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

IMETOLEWA NA

DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA


No comments:

Post a Comment

Adbox