Rais John Magufuli, kesho atapokea taarifa ya kazi ya uhakiki wa vyeti
kwa watumishi wa umma katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu imesema Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah
Kairuki ndiye atawasilisha taarifa hiyo kwa Rais.
Kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma iliendeshwa na Serikali kuanzia Oktoba mwaka jana.
Thursday, April 27, 2017
Wenye vyeti feki mikononi mwa Magufuli
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment