Watu 20 wafariki katka ghasia zilizozuka baina ya makabila mawili Kasai DR Congo
Watu 20 wameripotiwa kufariki kufuatia ghasia zilizozuka bain aya
makabila mawili katika mkoa wa Kasia Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Taarifa hiyo imetolewa Jumatano na ujumbe wa Umoja wa Mataifa MONUSCO.
Msemaji wa MONUSCO mjini Kinshasa Hag Serge katika mkutano na waandishi
wa habari alifahamisha kuwa watu 20 wa jamii ya Tshokwe-Pende
waliuawa Aprili 19 katika ghasia na jamii ya Lulua-Luba katika eneo la
Mungamba kwenye umbali wa kilomita 30 mashariki mwa Tshipaka.
Naibu gavana wa Kasai Jean-Hubert Mbingho hajathibitisha ghasia hizo
huku akikemea Umoja wa Mataifa kuonesha upendelevu katika taarifa yake.
No comments:
Post a Comment