Halmashauri ya Arusha mkoani hapa, wamepitisha mwongozo mpya wa mpango mkakati wa serikali,
kwa kipindi cha miaka mitano 2016/2020 kupitia Baraza maalumu la madiwani ,
mpango huo umelenga kupeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo ili kutatua kero
za wananchi hasa waliopo vijijini.
Akizungumza jana na waandishi wa habari
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Dokta Wilson Mahera alisema kuwa kwa
mujibu wa sheria ya mamlaka za serikali za mitaa ya mwaka 1982 kifungu 7 hadi
12 vimetoa uhalali wa uwepo wa serikali za mitaa sambamba na kutimiza wajibu
wake wa mpango mkakati (strategic plan)
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri
Noah Lembris alisema baraza kwa pamoja
wamefanya maanuzi yenye tija ya kuwapelekea wananchi maendeleo ya kweli bila
kujali itikadi ya vyama vyao.

No comments:
Post a Comment