Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeingia
matatani baada ya kushindwa kulipa deni sugu la shilingi bilioni 1.2,
inazodaiwa na mamlaka ya maji safi na Usafi wa mazingira (AUWSA) ,kutokana na
malimbikizo ya zaidi ya miaka 30 ya
malipo ya maji.
Mbali na jeshi hilo pia taasisi zingine za
serikali mkoani hapa ni Hospitali ya
mkoa, Mount Meru inayodaiwa zaidi ya sh,
milioni 700.1, shule ya sekondari ya Arusha sh milioni 67,Magereza ,Uhamiaji na
usalama wa Taifa.
Wadaiwa wengine ni Ikulu ndogo,ofisi ya
mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ,Jiji la Arusha, mashirika ya Umma na binafsi ,
Wateja wa majumbani na viwandani ambapo kwa ujumla Auwsa inadai kiasi cha shilingi billion 1.3.
Akizungumza jana na vyombo vya habari
jijini Arusha,mwenyekiti wa bodi wa Auwsa,Job Laizer aliwataka wadaiwa sugu
kujitokeza na kuanza kulipa madeni yao
mara moja kabla ya kuanza zoezi la kusitisha huduma ya maji mapema
iwezekanavyo.

No comments:
Post a Comment