![]() |
| Kenya inatumia mechi za kirafiki kujinoa kabla ya Kombe la CHAN 2018 |
Kocha wa timu ya
taifa ya soka nchini Kenya, Stanley Okumbi amewaita wachezaji 26 kambini
kwa minajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Angola tarehe 4 mwezi ujao.
Hata hivyo kikosi hicho kimewajumuisha wachezaji wanaocheza soka ya kulipwa nyumbani pekee. Wataripoti kambini mapema wiki ijayo kwa maandalizi zaidi.
Miongoni mwa wachezaji walioitwa kikosini ni;
Wadakaji: Boniface Oluoch (Gor Mahia), James Saruni (Ulinzi Stars), na Patrick Matasi (Posta Rangers)
Mabeki: Bolton Omwenga (Kariobangi Sharks), Haron Shakava (Gor Mahia), Titus Achesa (Posta Rangers), Jockins Otieno Atudo (Posta Rangers), Mayeko Musa Mohammed (Gor Mahia), Pascal Ogweno (Kariobangi Sharks), Robinson Mwangi Kamura (AFC Leopards), Simon Mbugua (Posta Rangers), Wilkison Marlon Tangauzi (Tusker)
Viungo: Ovella Ochieng (Kariobangi Sharks), Daniel Waweru (Ulinzi Stars), Duncan Otieno (AFC Leopards), Ernest Wendo (Gor Mahia), Jackson Macharia (Tusker), Kenneth Muguna (Gor Mahia), Samuel Onyango (Ulinzi Stars), Stephen Waruru (Ulinzi Stars), Victor Majid (Chemelil Sugar)
Washambulizi: Boniface Muchiri (Sony Sugar), Daniel Mwaura (Mathare United), Joseph Waithera (Wazito FC), Masita Masuta (Nzoia Sugar), Masoud Musa (Kariobangi Sharks)
Mchuano huo unajiri mwezi mmoja tu baada ya Kenya kutoka sare na Malawi katika mchuano wa kirafiki na uliohudhuriwa na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad.
Kenya itaandaa kombe la mataifa bora Afrika kwa wachezaji wa nyumbani, yaani CHAN mapema mwaka ujao.


No comments:
Post a Comment