![]() |
| FA imefikia uamuzi huo baada ya kushauriana na washikadau wa mchezo huo Uingereza |
Kuanzia msimu ujao,
wachezaji wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza wenye mazoea ya kusaka
penalti au mkwaju wa ikabu kupitia udanganyifu watachukuliwa hatua.
Kamati hiyo itawajumuisha mmoja wa wasimamizi wa mechi, meneja wa zamani na mchezaji wa zamani.
Mchezaji atakayepatikana kujirusha akisaka penalti, kupelekea utoaji wa kadi nyekundu au njano, ataadhibiwa kwa kupigwa marufuku na kukosa baadhi za mechi.
Shirikisho la soka nchini Uingereza FA, limefafanua kuwa madhambi hayo yatajulikana kama ''utapeli wa msimamizi wa mechi''.
Mabadiliko hayo mapya yalihitaji uungwaji mkono kutoka ligi kuu ya Premier nchini Uingereza, ligi ya daraja la chini, EFL na muungano wa wachezaji, PFA.
Wakati huo huo, FA imepitisha mabadiliko zaidi yakiwemo kutenga nafasi tatu kwa wanawake ifikapo 2018, kupuguza wanachama wa bodi hadi 10 na kuwashirikisha waanachama kumi na moja zaidi kuonyesha usawa.


No comments:
Post a Comment