shughuli za
benki, shule na vituo vya biashara zimesitishwa katika miji kadhaa ya
nchi hiyo ya magharibi mwa Africa
Taarifa zinasema kuwa, wanajeshi
waasi wanadhibiti maeneo muhimu ya miji
ya Yamoussoukro, San-Pédro, Bouaké na Abidjan katika hali ambayo, mkuu
wa majeshi ya nchi hiyo alikuwa amewataka wanajeshi hao waweke silaha
chini la sivyo wajiandae kukabiliwa na nguvu za jeshi. Wanajeshi hao
wameanzisha uasi wakilalamikia kucheleweshwa kulipwa malimbikizo yao ya
marupurupu.
| Wanajeshi waasi wa Ivory Coast |
Hii ni mara ya pili katika kipindi cha
miezi michache kushuhudiwa uasi wa wanajeshi nchini Ivory
Coast. Malalamiko ya uasi ya wanajeshi hao ambao wengi wao katika mji wa
Bouake walimsaidia Rais Ouattara kuingia madarakani yalianzia katika
mji huo ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo na kuenea hadi Abidjan
na miji mingine.
Mwezi Januari mwaka huu kulishuhudiwa uasi kama huo, hata hivyo ulifikia tamati baada ya mazungumzo ya maafisa wa ngazi za juu na wanajeshi hao waasi na ahadi za Rais Alassane Ouattara za kulipwa marupurupu wanajeshi hao, kupatiwa nyumba na kuongezewa mshahara. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, uasi wa mara hii wa wanajeshi ni wa kulalamikia kutotekelezwa ahadi zilizotolewa na Rais Alassane Ouattara.
Huku vuta nikuvute hiyo ikiendelea baina
ya wanajeshi waasi na serikali, nchi hiyo kwa sasa inakabiliwa na hali
mbaya ya uchumi unaolegalega huku raia wengi wa nchi hiyo ya magharibi
mwa Afrika wakilalamikia hali hiyo. Kuporomoka bei ya kakao ambalo ndilo
zao muhimu linaloipatia kipato nchi hiyo kutokana na kuuzwa nje ya
nchi, kunatajwa na wajuzi wa mambo kuwa, kumepelekea kupungua bajeti ya
nchi na matokeo yake ni kuchelewa kulipwa mishahara wanajeshi na
wafanyakazi wa baadhi ya idara za serikali.
| Rais Alassane Ouattara |
Aidha kufanyiwa marekebisho sheria ya
kustaafu kumeitwisha serikali mzigo mkubwa wa fedha huku mazingira
yakiwa magumu mno kwa wafanyakazi wastaafu. Ivory Coasti inakumbwa na
matatizo hayo katika hali ambayo, kuboreshwa hali ya uchumi, kuanzisha
nafasi za ajira na kupunguza umasikini ndizo zilizokuwa ahadi kuu za
Rais Alassane Ouattara katika kampeni zake za uchaguzi. Sio tu kwamba,
matatizo hayo hayajapatiwa ufumbuzi, bali filihali nchi hiyo inakabiliwa
na ukosefu wa uthabiti wa kisiasa.
Hata kama kufanyika uchaguzi na kupatikana usalama wa sasa wa nchi hiyo kunahesabiwa kuwa ni hatua moja kubwa ya kisiasa nchini Ivory Coast, lakini wapinzani nchini humo wamaendelea na harakati zao katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakitaka Rais Alassane Ouattara ajiuzulu na kuachia ngazi.
Hivi sasa kutokana na nchi hiyo kuwahi
kushuhudia mapinduzi ya kijeshi, kumezuka wasiwasi wa kukaririwa tena
tukio kama hilo nchini humo. Licha ya kuwa wanajeshi waasi wametangaza
wazi kwamba, wako pamoja na Rais Alassane Ouattara na wanachodai wao ni
kuboreshwa tu hali yao, lakini mvutano wa sasa umeongeza wasiwasi wa
kutokea mapinduzi katika nchi hiyo.
Aidha uwepo wa makundi ya kigaidi katika
maeneo mbalimbali ya bara la Afrika kumeongeza wasiwasi wa kupanuka
harakati za makundi ya kigaidi katika nchi ambazo zinakabiliwa na
machafuko na migogoro.
Kwa sasa jambo la msingi ni wawakilishi
wa serikali kufikia makubaliano na wanajeshi hao waasi ili kuzuia nchi
hiyo kutumbukia tena katika vita na machafuko ya ndani.

No comments:
Post a Comment