Jeshi
la polisi kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa Singida limeanzisha
zoezi kambambe la kukagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi huku
likisisitiza kuwa zoezi hilo kuwa endelevu.
Akizungumza kwa
niaba ya kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida, RTO Mrakibu wa
Polisi Peter Raphael Majira, amesema zoezi hilo lililoanza jana
litaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa Singida.
Amesema lengo
ni kuhakikisha mabasi hayo yanakidhi mahitaji yote ya sheria za usalama
barabani, wakati wote yanapokuwa barabarani.
Amesema pia
wanatoa elimu na wanawakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo, juu
ya wajibu wao na umuhimu wa kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za
usalama barabarani.
Aidha
RTO Peter amesema wanawakumbusha madereva kujenga utamaduni wa kuwa na
tahadhari zaidi na kitendo hicho kitapunguza kwa kiwango kikubwa ajali
za barabarani.
Pia ametumia fursa hiyo kuwataka wenye watoto
wanaotumia mabasi hayo wahakikishe mtoto anakaa kwenye kiti chake na si
kuchangia kiti.
“Mzazi/mlezi usikubali kabisa mwanao achangie
kiti, umelipitia kiti kwa nini achangie na wanafunzi mwingine. Na ninyi
wamiliki wa mabasi haya kama kuna hafla wanafunzi wanakwenda kuhudhuria
iwapo wamejaa (yaani kila mwanafunzi ana kiti chake), peleka hao
waliopata viti halafu urudie wengine” amesisitiza mrakibu Peter.
Askari wa usalama barabarani mkoani Singida, E.8763. Sgt. Benes Lucas akikagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi mjini hapa jana.
Baadhi ya mabasi kati ya 20 yanayotumika kusafirisha wanafunzi Mkoani Singida yakifanyiwa ugazi na askari usalama barabarani kwa lengo la kujiridhisha ubora wake.
RTO Mkoa wa Singida Mrakibu wa polisi Peter Raphael Majira akitoa taarifa ya zoezi la ukaguzi wa mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi kwa lengo la kukagua ubora na pia kuwakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo juu ya sheria za usalama barabarani.
zoezi kambambe la kukagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi huku
likisisitiza kuwa zoezi hilo kuwa endelevu.
Akizungumza kwa
niaba ya kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida, RTO Mrakibu wa
Polisi Peter Raphael Majira, amesema zoezi hilo lililoanza jana
litaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa Singida.
Amesema lengo
ni kuhakikisha mabasi hayo yanakidhi mahitaji yote ya sheria za usalama
barabani, wakati wote yanapokuwa barabarani.
Amesema pia
wanatoa elimu na wanawakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo, juu
ya wajibu wao na umuhimu wa kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za
usalama barabarani.
Aidha
RTO Peter amesema wanawakumbusha madereva kujenga utamaduni wa kuwa na
tahadhari zaidi na kitendo hicho kitapunguza kwa kiwango kikubwa ajali
za barabarani.
Pia ametumia fursa hiyo kuwataka wenye watoto
wanaotumia mabasi hayo wahakikishe mtoto anakaa kwenye kiti chake na si
kuchangia kiti.
“Mzazi/mlezi usikubali kabisa mwanao achangie
kiti, umelipitia kiti kwa nini achangie na wanafunzi mwingine. Na ninyi
wamiliki wa mabasi haya kama kuna hafla wanafunzi wanakwenda kuhudhuria
iwapo wamejaa (yaani kila mwanafunzi ana kiti chake), peleka hao
waliopata viti halafu urudie wengine” amesisitiza mrakibu Peter.

No comments:
Post a Comment