LATEST NEWS

Thursday, May 18, 2017

Serengeti Boys yawatoa kimasomaso Watanzania



Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imewatoa kimasomaso Watanzania mara baada ya kuwaduwaza vijana wenzao wa Angola kwa kuwachapa kwa mabao 2-1 katika pambano lililokuwa gumu na la kuvutia.

 Serengeti walianza pambano hilo kwa kasi na kufanikiwa kupata goli mapema kupitia kwa Kelvin Nashon dakika ya 5 akiunganisha vyema krosi iliyotokea winga ya kulia. Angola walisawazisha bao hilo dakika ya 20 baada ya mabeki wa Serengeti kushindwa kuundoa mpira uliokuwa unazagaa golini kwao. hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Serengeti Boys ndio waliotengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia hadi ilipotimu dakika ya 68 ambapo Serengeti Boys walipata goli la pili na la ushindi.

Usiku huu bingwa wa michuano hiyo Mali watavaana na Niger. 
Tanzania

No comments:

Post a Comment

Adbox