LATEST NEWS

Sunday, May 28, 2017

MAKALA YA SHERIA: UWEZEKANO WA KUYASHITAKI MAKAMPUNI YA MADINI KUREJESHA HASARA TULIYOIPATA HUU HAPA.



Na Bashir Yakub

Mikataba yote ya kimataifa huongozwa na
wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao
haukuandikwa(implied obligation).

Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya
mkataba yaliyo katika maandishi ambayo wahusika husoma na kuridhia,
wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika
mkataba lakini yapo kwa asili au yapo kwa kuwa tayari yalishasemwa na
sheria na hivyo si lazima kuyaandika katika mkataba.

Mathalan, mfanyakazi wako wa duka
hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la
uaminifu. Laa hasha uaminifu ni sharti la asili "implied
obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe bado lipo tu.Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya
kwetu na makampuni ya madini masharti yafuatayo ni ya asili na
hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :


1.
Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu  shughuli inayotekelezwa
katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the
subject matter). 

2.
Wajibu wa kutekeleza na kutenda  kwa nia njema(Implied covenant to act in
good faith and fair dealing). 

3.
Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa  mkweli . Hili huwa ni katazo
la udanganyifu(Fraud). 

Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au
hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri  yake ni kukiuka masharti ya mkataba.

Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa
madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua
zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata
na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu na masharti ya mkataba jambo ambalo
ni kinyume cha sheria. Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi
hiyo basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo.

No comments:

Post a Comment

Adbox