Wednesday, May 24, 2017

Polisi watatu wauawa katika mlipuko uliotokea eneo la mpaka wa Kenya

Askari polisi watatu wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa hii leo wakati gari lao lilipokanyaga bomu lililotegwa ardhini kwenye kaunti ya Garissa nchini Kenya.

Ofisa serikali wa eneo hilo Mohamud Saleh amesema, tukio hilo limetokea wakati askari polisi hao walipokuwa wakisafiri kuelekea mji wa Liboi katika eneo la mpaka kati ya Kenya na Somalia wakitokea eneo la Kulan.

Bw. Saleh amesema wapiganaji wa kiislamu wanazunguka kwenye eneo hilo baada ya vikosi vya usalama vya serikali kuongeza ulinzi katika eneo la mpaka.

Tukio hilo limetokea wiki moja baada ya gari lingine kukanyaga bomu katika eneo hilohilo na kusababisha vifo vya watu wanne, akiwemo mtoto wa mwaka mmoja. 


Source:CRI
 

No comments:

Post a Comment

Adbox