Watu 17 wafariki na wengine kujeruhiwa katika ajali ya barabarani mashariki mwa Zambia
Watu 17 wamefariki na wengine 48 kujeruhiwa wakati basi lililokuwa likitokea kwenye mji mkuu wa Zambia, Lusaka, kupoteza mwelekeo na kupinduka.Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Esther Mwaata-Katongo amesema, ajali hiyo imetokea jana majira ya saa tatu usiku kwa saa za huko baada ya dereva wa basi kushindwa kukata kona, na kusababisha basi hilo kupinduka. Amesema miongoni mwa marehemu ni watoto watatu, wanaume sita na wanawake watatu.
Ajali za barabarani hutokea mara kwa mara nchini Zambia, ambapo mwaka jana, serikali ilipiga marufuku magari yote kusafiri usiku ili kupunguza ajali hizo.
No comments:
Post a Comment