Waziri Mkuu wa
Tanzania Kassim Majaliwa amewataka watanzania wote kutunza miundombinu yote
inayojengwa kwa ajili yao ili kuleta maendeleo.
Waziri Mkuu ameyasema
hayo leo wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Arusha-Holili . Ujenzi huo kwa
sasa upo katika awamu ya kwanza yaani barabara ya urefu wa kilomita KM 14 kwa
kiwango cha lami kutoka Sakina hadi Tengeru.
Akizungumza kabla ya
kumkaribisha Waziri Mkuu, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alimueleza Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa,kuwa viongozi wa vijiji wengi wameshiriki kuuza maeneo ya wananchi
kiasi kwamba hata serikali inashindwa kupeleka huduma kwa wananchi kwa wakati
hususani huduma za kiafya kama zahanati.














No comments:
Post a Comment