LATEST NEWS

Thursday, May 4, 2017

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani hapa limeanza operesheni ya kukata umeme kwa wadaiwa sugu.

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani hapa limeanza operesheni ya kukata umeme kwa wadaiwa sugu. 

Akizungumza baada ya operesheni hiyo, Ofisa Uhusiano wa Tanesco, Saidy Mremi amesema wamelazimika kukata umeme ili walipwe madeni yao ambayo ni zaidi ya Sh8 bilioni. “Taasisi za Serikali tunazidai asilimia 28 ya deni hilo ambapo tumeamua kuanza nao,”amesema.

Utekelezaji huo umekuja ikiwa imepita takriban miaka miwili tangu Rais John Magufuli atoe agizo la kulitaka shirika hilo kuwakatia umeme wadaiwa sugu.

No comments:

Post a Comment

Adbox