LATEST NEWS

Friday, June 16, 2017

BALOZI MASIMA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA TAIFA LA ISRAEL

Katika sherehe hiyo, Rais Rivlin alimshukuru Mhe. Dr John Pombe Joseph Magufuli, kwa kumteua balozi mkazi wa kwanza ubalozi nchini Israel . Ampongeza pia kwa hatua mbali mbali anazozichukua katika kukukuza uchumi na kusifia serikali yake kwa kudumisha hali ya utulivu na amani nchini Tanzania. Kwamba anaiona nchi ya Tanzania ikiwa yenye maendeleo makubwa mbeleni chini ya uongozi wake. Kwa upande wake, pamoja na mambo mengine, balozi aliwasilisha salamu maalimu za Rais Magufuli kwa Rais Ruvlin, serikali na wananchi wa Israel na kuahidi kudumisha mahusiani yaliyopo na yenye historia kubwa. Ubalozi wa Tanzania umepewa usajili wa kibalozi namba 88. Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akipokewa kwa nyimbo za taifa baada ya kuwasili kwenye Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa taifa hilo Mhe. Reuven Rivlin
Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akijitambulisha kwa Rais wa taifa hilo Mhe. Reuven Rivlin kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho
Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akiwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel Mhe. Reuven Rivlin Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem
Akiwa amevaa baragashia ya kitamaduni ya Kiyahudi maarufu kama "Kippah" Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima akiwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na kusoma salamu maalumu za mwanzo wa urafiki mpya wa ushirikiano wa karibu kwa ki-Hebrew baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel Mhe. Reuven Rivlin Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem.

Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima akikaribishwa rasmi baada ya kuwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na kusoma salamu maalumu za mwanzo wa urafiki mpya wa ushirikiano wa karibu kwa ki-Hebrew baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel Mhe. Reuven Rivlin Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem.

Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima akikaribishwa rasmi kwa toast baada ya kuwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na kusoma salamu maalumu za mwanzo wa urafiki mpya wa ushirikiano wa karibu kwa ki-Hebrew baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel Mhe. Reuven Rivlin Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem.

Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima akiwa katika mazungumzo na Rais wa Taifa la Israel Mhe. Reuven Rivlin Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem.

No comments:

Post a Comment

Adbox