LATEST NEWS

Tuesday, June 27, 2017

FIFA Kombe la mabara: Ujerumani na Chile zafuzu nusu fainali.

Ujerumani na Chile zimetinga nusu fainali ya mashindano ya FIFA kombe la mabara baada ya kumaliza mechi zao za kundi B.

Ujerumani wametwaa ushindi wa kundi B baada ya kuichapa Cameroon 3-1 huku Chile wakishika nafasi ya pili baada ya kutoka sare ya 1-1 na Australia,

Jumatano ijayo, Ureno itaivaa Chile kwenye nusu fainali ya kwanza huko Russia na Ujerumani kukutana na Mexico siku ya Alhamis kwenye nusu fainali ya pili.

No comments:

Post a Comment

Adbox