Bondia Francis Cheka amechezea kipigo toka kwa bondia mwenzake Enes Zecirevic katika pambano lililofanyika jumapili mjini Geneva Uswisi.
Cheka alipigwa kwa pointi za majaji 3-0 kwenye pambano hilo la raundi 8 la uzani mwepesi wa juu (kg 81).
Cheka amesema asingeweza kushinda kwa pointi kwasababu alijua matokeo yale baada ya kumaliza raundi zote huku akijitetea kuwa mabondia wageni wanapocheza ugenini na kumaliza raundi zote ni vigumu kupewa ushindi dhidi ya mwenyeji.
No comments:
Post a Comment