Agosti 8 Jose Mourinho sasa ataiongoza timu yake Manchester United kuivaa timu yake ya zamani mabingwa wa UEFA Champions Ligi Real Madrid kwenye mechi ya kuanua msimu mpya wa mashindano ya klabu bingwa ulaya katika mechi ya UEFA Super Cup.
UEFA SUPER CUP hugombewa kila mwaka na washindi wa UEFA Champions Ligi na wale wa UEFA Europa Ligi.
Mechi hii ya fainali itachezwa katika uwanja wa Phillip II Arena mjini Skopje nchini Macedonia, ni uwanja ambao unachukua watu 33,000. Nchi hii inapakana na nchi za Bulgaria, Serbia, Albania na Greece. Na hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Macedonia kuwa mwenyeji wa fainali kubwa ya ulaya.
No comments:
Post a Comment