LATEST NEWS

Monday, June 26, 2017

Uongozi wa Yanga walaani kitendo cha mashabiki kuchoma moto jezi ya Niyonzima





Image result for jezi namba 8 niyonzima 

Uongozi wa Yanga umelaani kitendo cha mashabiki wachache wa Yanga kuchoma jezi namba 8 iliyokuwa inavaliwa na kiungo Haruna Niyonzima.

Wiki iliyopita, Yanga kupitia Katibu wake Mkuu, Charles Boniface Mkwasa ilitangaza rasmi kumuachia Niyonzima raia wa Rwanda kuendelea na maisha yake kutokana na kutaka dau kubwa.

Siku chache baada ya kauli hiyo, ikaonekana baadhi ya mashabiki wakichoma jezi za kiungo huyo Mnyarwanda wakionyesha hasira zao kutokana na uamuzi wake wa kuamua kuondoka na kwa kuwa ameanza mazungumzo na Simba.

No comments:

Post a Comment

Adbox