LATEST NEWS

Monday, June 26, 2017

COSAFA 2017: Tanzania yaanza vyema

Tanzania imeanza vyema mashindano ya COSAFA 2017 huko Moruleng Afrika Kusini kwa kuifunga Malawi 2-0 katika mechi ya kundi A. Magoli ya Taifa Stars yalifungwa na Ramadhan Shiza Kichuya katika dakika ya 13 na 18. 

Kwenye mashindani hayo Tanzania ipo kundi A pamoja na Angola, Mauritius na Malawi. Na kundi B lina timu za Zimbabwe, Madagascar, Mozambique na Sychelles.
Nchi nyingine wanachama wa COSAFA, Afrika Kusini, Swaziland, Botswana na Zambia wataanzia hatua ya robo fainali.

No comments:

Post a Comment

Adbox