Kikosi cha wanasoka 20 kutoka timu za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) kitazuru Uhispania kuanzia Jumatatu hadi Julai 25 kwa mechi mbili za kirafiki dhidi ya klabu za taifa hilo.
Taarifa fupi kutoka makao makuu ya Shirikisho la Soka (FKF) ilisema waandaaji wa ziara hiyo, La Liga wamegharamia safari hiyo pamoja na malazi. Habari hizo zilisema timu hiyo itakayojulikana kama KPL All Stars itakuwa chini ya kocha Stanely Okumbi akisaidiwa na John Kamau.
No comments:
Post a Comment