Bao pekee la mshambuliaji Elius Maguri limetosha kuipeleka Tanzania nusu fainali ya michuano ya kombe la COSAFA baada ya kuwalaza wenyeji bao 1-0 jana kwenye uwanja wa Royal Bafokeng Afrika Kusini.
Maguri alifunga bao hilo dakika ya 18 kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ndefu ya kiungo Muzamil Yassin.
Tanzania sasa itakutana na Zambia katika nusu fainali itakayopigwa jumatano.
No comments:
Post a Comment