LATEST NEWS

Thursday, July 27, 2017

IGP SIRRO AFANYA ZIARA MKOANI SIMIYU

  

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiweka saini kwenye kitabu cha
wageni wakati alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka,
kwa lengo la kujitambulisha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo,
IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi na kuzungumza na askari wa Jeshi
hilo.



Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la
Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, ambaye amefika katika ofisi yake kwa lengo la
kujitambulisha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, IGP Sirro yupo
mkoani humo kwa ziara ya kikazi na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo, kulia ni
kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Boniveture
Mushongi.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya
wananchi wa Mwamapalala mkoani Simiyu, wakati akiwa njiani kuelekea mkoani
Shinyanga, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari wa Jeshi hilo
pamoja nakujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao.



Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya
wananchi wa Maganzo mkoani Shinyanga, wakati alipowasili akitokea mkoani
Simiyu kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari wa Jeshi hilo
pamoja nakujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu. Picha
na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Adbox